Sun. Apr 20th, 2025

Kilichomuua William Kamoti Mbunge wa Rabai

Mbunge wa Rabai William Kamoti Mwamkale ameaga dunia usiku wa kuamka leo baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani maeneo ya Komaza kwenye barabara kuu ya Kilifi kuelekea Mombasa.

Akithibitisha kisa hicho Kamanda wa Polisi eneo hilo Jonathan Koech amesema ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa tatu usiku, ilitokea baada ya dereva kujaribu kukwepa gari lilokuwa likiendeshwa kwa kasi.

Koech anasema dereva alipoteza muelekeo na kupelekea gari hilo la mjumbe huyo kubingiria mara kadhaa na kupelekea kifo cha Kamoti.

Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amemtaja Kamoti kama kiongozi shupavu aliyapa maslahi ya wananchi kipaumbele.

Mwambire anasema kifo chake ni pigo kubwa cha chama hicho akisema kifo chake kilitokea alipokuwa ametoka kuidhinishwa na tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC. 

Kamoti alikuwa mjumbe wa kwanza tangu eneo bunge la Rabai kuundwa, akichaguliwa kupitia kwa chama cha ODM. 

Mwili wa mwendazake utazikwa hii leo nyumbani kwake kule Rabai baada ya Swalat ya saa Kumi.

By Treeza Auma

Treeza Auma is a Digital Content Producer and founder of https://www.ktmn.co.ke KTMN She is also Television journalist at Kenya News Agency and Leadership Accelerator at Women in News.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *