Polisi mjini Kilifi wanamzulia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kuwahonga wapiga kura katika kituo cha kupiga kura cha shule ya msingi ya Kibaoni.
Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Nelson Taliti, amesema mwanamke huyo amekamatwa akiwa na kitita cha pesa takriban shilingi elfu 25.
Taliti amesema kuwa elfu ishirini ya pesa hizo zilikuwa ni noti za shilingi mia moja huku shilingi elfu Tano ni noti za shilingi hamsini.
Duru za kuaminika zinasema kuwa mwanamke huyo anajihusisha na Chama Cha Pamoja African Alliance (PAA).
Kwa upande wake mgombea wa ubunge wa Kilifi Kaskazini kwa chama cha ODM Eliud Kalama, amekashifu kitendo hicho akisistiza kwamba ni ukiukaji wa demokrasia.
Aidha ameziomba asasi za usalama kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaopatikana na kosa hilo.